DRC-MAUAJI-USALAMA

Makaburi 8 ya halaki yagunduliwa karibu na mji wa Tshimbulu, DRC

Kaburi la halaiki karibu na mji wa Tshimbulu, DRC.
Kaburi la halaiki karibu na mji wa Tshimbulu, DRC. RFI/Sonia Rolley

Hii ni moja ya ushahidi wa vurugu zinazoshuhudiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu katika mkoa wa Kasai ya Kati, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. RFI na Reuters wamefanya uchunguzi wa kugundua makaburi 8 ya halaiki karibu na Tshimbulu, mji mkuu wa wilaya ya Dibaya.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa uliwasilisha kwa serikali ya DR Congo taarifa kuhusu makaburi matatu ya halaiki karibu na mjiji huo, ambao kwa muda mrefu umekumbwa na mapigano yaliyosababoshwa na kiongozi wa kikabila, Kamuina Nsapu.

"Hapa tuko kwenye makaburi lililochimbwa na askari DR Congo, wala haijulikani idadi ya watu waliozikwa hapa," amesema mkazi mmoja wa Tshimbulu. Hii si mara ya kwanza mtu huyu kutembelea eneo hili, kilometa chache mji wa Tshimbulu, kando ya barabara. Majani marefu yaliweza kuzuiwa wapita njia kugundua eneo hilo. "Asubuhi tulikwenda shambani. Tulipofika, tuliona nzi wengi wakiruka na kulikuwa na harufu kali, " ameleza shahidi. Yeye, miongoni mwa wengine, walijaribu kuingia katika eneo hilo na kugundua shimo la upana wa mita tano kwa urefu wa kumi, ambalo lilifunikwa vibaya. "Tuliona mikono, miguu na hata miili mizima, watu waliouawa walizikwa vibaya," alisema mtu huyo, akionyesha mifupa ya binadamu ambayo bado inaonekana eneo hilo.

RFI/Sonia Rolley

Mkazi huyu wa Tshimbulu kama mashahidi wengine wanasema waliona wanaume, wanawake na hata watoto. Walikuwa wamezikwa katika mashimo kumi na tatu, shimo la kumi nne ndilo lilikua wazi. Kaburi kubwa ambalo lilikua na maiti moja pekee. Wakazi wa Tshimbulu wameeleza kwamba Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Dr Congo (MONUSCO) walipiga picha ya kaburi hilo la halaiki, na lingine la pili linalopaikana kando ya barabara kilometa na eneo kulikogunduliwa kaburi la kwanza.

Makaburi ya halaiki yasiopungua manane yamegundulika na wakazi wa Tshimbulu tangu mwanzoni wa mwaka huu.

RFI/Sonia Rolley