DRC-ICC

ICC yasema watu 297 waliovamiwa na waasi wa Germain Katanga watafidiwa

Germain Katanga
Germain Katanga jfjustice.net

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, imeagiza kulipwa fidia kwa watu 297 waliothirika baada ya kuwavamiwa na waasi wa FRPI waliongozwa na Germain Katanga katika kijiji cha Bogoro mkoni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Majaji wa Mahakama hiyo wamesema kuwa kila mwathiriwa atapata Dola za Marekani 250 kutokana na uvamizi huyo mwaka 2003.

Aidha, imeamuliwa kuwa Katanga ambaye anakitumikia kifungo cha miaka 12 jela, atatoa Dola Milioni 1 ili kufanikisha malipo hayo.

Kiasi cha dola Milioni 3.7 zinahitajika ili kuwafidia watu hao.

Katanga mwenye umri wa miaka 38, ambaye pia anaitwa Simba, alipatikana na kosa la kuongoza mauaji, ubakaji na kuwafanya raia aliowateka kuwa watumwa.