UFARANSA-CHAD

Raia wa Ufaransa atekwa nyara nchini Chad

Ramani ya nchi ya Chad inayokaribiana na Libya
Ramani ya nchi ya Chad inayokaribiana na Libya Wikipedia

Serikali ya Ufaransa imesema raia wake ametekwa nyara nchini Chad, katika ukanda wa Afrika ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa utekaji nyara huo ulitokea katika mji wa Abeche Mashariki mwa nchini hiyo lakini taarifa zaidi hazijaelezwa.

Taarifa za kijeshi kutoka Paris zinasema serikali zote mbili zimeweka mikakati ya kumtafuta na kumwokoa mateka huyo.

Raia kadhaa wa Ufaransa na wengine kutoka mataifa mengine ya Afrika Magharibi, wamekuwa wakitekwa na makundi ya kijihadi katika nchi za Afrika Magharibi na Kati.

Mara ya mwisho kwa raia wa Ufaransa kutekewa ilikuwa ni mwaka 2009 lakini akaachiliwa huru baada ya siku 89.

Visa hivi vimekuwa vikiendelea licha ya jeshi la Ufaransa kuwa nchini humo katika operesheni iliyofahamika kama Barkhane, kukabiliana na makundi ya kigaidi kama Al-Qaeda.

Hadi sasa raia wa pekee wa Ufaransa anayefahamika kwa jina la Sophie Petronin, kutokana na kazi zake za kijamii na bado anatafutwa baada ya kutekwa mjini Gao nchini Mali mwaka uliopita.