ICC

Raia wa Zambia kuanza mjadala kuhusu kujiondoa ICC

Jengo la mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC.
Jengo la mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC. REUTERS/Jerry Lampen/File Photo

Zambia imeanza mjadala ikiwa itajiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umechukuliwa na Wizara ya Haki nchini humo baada ya kutuma taarifa kituo cha taifa nchini humo.

Majadiliano hayo yanatarajiwa kuafanyika katika Wilaya zote 30 kuanzia siku ya Jumatatu wiki ijayo.

Wachambuzi wa siasa wanasema hakuna haja yoyote ya Zambia kujiondoa katika Mahakama hiyo na inavyoonekana, inapata shinikizo kutoka nje ya nchi.

Viongozi wa bara la Afrika, wamekuwa wakidai kuwa Mahakama ya ICC inawalenga viongozi wa Afrika lakini madai hayo yamekuwa yakikanusha na Majaji wa Mahakama hiyo.

Mataifa mengine ya Afrika ambayo yamewahi kuonesha nia ya kujiondoa katika Mahakama hiyo ni pamoja na Burundi, Afrika Kusini na Gambia.

Hata hivyo, Mahakama ya Afrika Kusini jijini Pretoria imeagiza serikali nchini humo kuachana na mpango wa kujiondoa katika Mahakama hiyo kwa sababu ni kinyume cha Katiba ya nchi hiyo.

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow naye amesema nchi yake haitaondoka katika Mahakama hiyo.