DRC-USALAMA
Polisi 40 wauawa Kasai DRC
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kundi la wapiganaji wa Kamwina Nsapu nchini DRC limetekeleza mauaji ya maafisa 40 wa polisi katika shambulizi jimboni kasai,maafisa katika eneo hilo wamearifu.
Matangazo ya kibiashara
Shirika la habari la Uingereza BBC Limeripoti kuwa wapiganaji wa kundi la Kamwina Nsapu walishambulia msafara wa maaskari hao.
kiongozi wa Kasai Francois Kalamba ameeleza kuwa askari sita waliachiwa huru lakini wengine walichinjwa.
Machafuko katika jimbo la Kasai yalianza mnamo mwezi August mwaka jana baada ya vikosi vya usalama kumuua kiongozi wa kundi hilo la Kamwina Nsapu.