Mjadala wa Wiki

Maaskofu nchini DRC wasema wanasiasa hawana nia ya kutekeleza mkataba wa kisiasa

Sauti 15:20
Mwenyekiti wa baraza la maaskofu wa kanisa Katoliki, Cenco; Askofu mkuu Marcel Utembi, na katibu mkuu wa Cenco, Donatien Nsholé, Desemba 30 2016 jijini Kinshasa DRC.
Mwenyekiti wa baraza la maaskofu wa kanisa Katoliki, Cenco; Askofu mkuu Marcel Utembi, na katibu mkuu wa Cenco, Donatien Nsholé, Desemba 30 2016 jijini Kinshasa DRC. scd.sw.rfi.fr

Baraza la maaskofu nchini DRC limewasilisha ripoti kuhusu mazungumzo ya kisiasa yaliyofanyika mwaka uliopita na kufikia mkataba wa kuundwa kwa serikali ya mpito kuelekea Uchaguzi Mkuu mwishoni mwa mwaka huu.Maaskofu hao wameelezea masikitiko yao kuhusu utekelezwaji wa mkataba huo ambao hadi sasa bado unazua mvutano kati ya serikali na upinzani.Suala la uteuzi wa Waziri Mkuu linasalia kuwa tata. Victor Abuso anachambua hili na Mbunge wa serikali Didier Manara na Mwandishi wa RFI Kiswahili Ali Bilal.