TANZANIA-ETHIOPIA

Waziri mkuu wa Ethiopia ziarani nchini Tanzania

Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ambaye anaanza ziara ya kikazi nchini Tanzania
Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ambaye anaanza ziara ya kikazi nchini Tanzania Photo: Reuters/Tiksa Negeri

Waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn hii leo anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania, ambapo pamoja na mambo mengine yeye na mwenyeji wake rais John Pombe Magufuli, wanatarajia kutiliana saini mikataba kadhaa ya ushirikiano wa kiuchumi na biashara.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu Desalegn, atawasili jijini Dar es Salaam saa tatu na nusu asubuhi kwa saa za hapa Afrika mashariki ambapo atapokelewa na mwenyeji wake rais Magufuli na kisha kuelekea ikulu kwa mazungumzo kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari.

Kiongozi huyo wa Ethiopia atatamatisha ziara yake kesho mchana kwa kutembelea bandari ya Dar es Salaam.

Wachambuzi wa mambo wanaitazamaje ziara hii? Haji Kaburu ni mchambuzi wa siasa za kimataifa anazungumza nasi akiwa jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Haji Kaburu Mchambuzi wa masuala ya siasa za Kimataifa

Ziara ya waziri mkuu Hailemariam Desalegn, imekuja ikiwa ni miezi michache imepita toka rais Magufuli ahudhurie mkutano wa wakuu wa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia.