DRC-UN

UN yaongeza muda wa MONUSCO DRC

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura.
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura. UN Photo/Loey Felipe

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linaloongeza muda wa ujumbe wa umoja huo MONUSCO nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kupunguza idadi ya askari wake.

Matangazo ya kibiashara

MONUSCO imeongezewa muda hadi tarehe 31 mwezi Machi mwakani.

Kwa mujibu wa umoja wa mataifa azimio hilo limegusia suala muhimu lililokuwa linajadiliwa kuhusu kupunguza idadi ya askari, ambapo sasa imepunguzwa hadi askari 16,215.

Azimio limemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kufanya tathmini ya majukumu ya MONUSCO kwa wakati huu kuona iwapo majukumu yote ni muhimu.

Wanachama wa baraza hilo wamemuonya raisi Joseph Kabila kwamba utawala wake lazima iheshimu mkataba wa kusirikiana uongozi na upande wa upinzani na kuruhusu uchaguzi muhimu kufanyika.

Balozi wa uingereza katika baraza la usalama la umoja wa mataifa Matthew Rycroft, ambaye alikuwa mwenyekiti wa baraza mwezi huu ameeleza kuwa ukosefu wa usalama na mvutano umeendelea kushuhudiwa katika kipindi chote nchini DRC.