AFRIKA-INDIA

India yakanusha madai ya kuwalinda raia wake wanaowashambulia waafrika

Baadhi ya raia kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakiandamana katika mji wa Hyberabad tarehe 6 Februari mwaka 2016
Baadhi ya raia kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakiandamana katika mji wa Hyberabad tarehe 6 Februari mwaka 2016 AFP/Noah SEELAM

Serikali ya India imekanusha madai kutoka kwa mataifa 44 ya bara Afrika kuwa, imeshindwa kuwalinda Waafrika hasa wanafunzi wanaoendelea kushambuliwa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya pamoja kutoka Mabalozi wa mataifa hayo, imeishutumu serikali ya India kwa kutowachukulia hatua raia wake wanaotuhumiwa kutekeleza mashambulizi hayo.

Hata hivyo, New Delhi imesema madai ya Mabalozi hayo hayakubaliki na ripoti za kushambuliwa kwa raia wa Nigeria hivi karibuni zinachunguzwa, na hatua itachukuliwa.

Mabalozi hao wanasema mashambulizi dhidi ya raia wa Afrika ni ya ubaguzi wa rangi, na hayakubaliki kamwe.

Pamoja na hayo, raia wa India wamemshutumu raia wa Nigeria kumteka mtoto wa Kihindi na kumuua wiki iliyopita nje ya jiji kuu New Delhi.

Hata hivyo, polisi walipata mwili wa mtoto huyo na kusema kuwa raia wa Nigeria hawakuhusika kwa vyovyote vile kwa madai ya kulipiza kisasi.