BENIN - BUNGE

Bunge la Benin lapiga kura ya hapana kupinga marekebisho ya katiba

Muandamanaji wa kike mbele ya majengo ya bunge la kitaifa mjini Porto Novo,  4 avril 2017.
Muandamanaji wa kike mbele ya majengo ya bunge la kitaifa mjini Porto Novo, 4 avril 2017. YANICK FOLLY / AFP

Wabunge nchini Benin kwa mshamgano mkubwa wamepiga kura ya hapana kupinga muswada wa marekebisho ya katiba kama ilivyopendezwa na rais wa nchi hiyo Patrice Talon. hivyo muswada huo wa marekebisho ya katiba hautojadiliwa tena. Ilitakiwa kura 63 ili kupasisha muswada huo, ambapo wabunge 63 walipiga kura ya ndio huku 22 wakapiga kura ya hapana na mwingine mmoja akashindwa kubaini msimamo wake. zimekosekana kura 3 pekee ilikuidhinisha muswada huo. hili ni pigo la pili kwa kwa rais Talon baada ya wabunge kupinga pendekezo la rais la kujadili kwa dharura muswada wa marekebisho ya katiba.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mambo yanayotaka kurekebishwa katika katiba hiyo, ni pamoja na kubadili muhula wa rais kutoka muhiula miwili hadi mmoja.

Kwa mujibu wa mbunge Guy Mitokpè, amesema kujadili swala hilo la marekebisho ya katiba sio kipao mbele katika kipindi hiki, na kwamba huu ni ushindi wa wananchi, sio ushindi wa kundi hili au lile, na sio ushindi dhidi ya mtu. Kwa sasa inabidi kupanga muswada huo na kuendelea na mambo mengine muhimu, ameendelea kusisitiza.

kwa muda wa saa tatu za majadiliano, wapinzani wametoa rai tatu muhimu: Kuna maswala ya kijamii na kiuchumi ambayo yanatakiwa kupewa kipao mbele mbali na muswada wa marekebisho ya katiba, inabidi kuanzisha mchakato utaoshirikisha pande zote wakiwemo raia wa nchi hiyo na kwamba muswada huo hauwezi kukubalika kwa namna ulivyo kwa sasa.

Waziri wa sheria Joseph Djogbenou, aliekuwepo bungeni kuutetea muswada huo amesema Benin imepoteza fursa muhimu sana ya kubadili sheria ya msingi, na kwamba kuna umuhimu wa kufanya marekebisho ya katiba hiyo na kwamba anaimani ipo siku raia wa nchi hiyo watafaulu kuifanyia marekebisho, labda sio kwa kipindi hiki.

Mbele ya ofisi za bunge kundi la watu walijitokeza kuandamana kusherehekea ushindi huo akiwemo Pascal alitoka mbali kuja kusema hapana kuhusu marekebisho ya katiba na kwamba katiba iliopo ilipatikana kwa maelewano na wananchi ndio waliopendekeza ni ushindi wa wananchi dhidi ya pesa za rais Talon.

Mjadala pia ilikuwepo kuhusu pesa. Mbunge Rosine Soglo mwenye umri wa miaka 83 amethibitisha kupokea pesa, baada ya upigaji kura, viongozi wa tume 5 za wabunge walimtaka aombe radhi, jambo ambalo ametupilia mbali.