DRC na Rwanda zakubaliana kutafuta mafuta katika Ziwa Kivu
Imechapishwa:
Wizara za Mambo ya nje nchini humo zinasema kuwa hatua hii ina maanisha kuwa uhusiano kati ya nchi hizi mbili zinapakana na Ziwa hilo, ni nzuri na imara.
Waziri anayehusika na maswala ya mafuta nchini Rwanda Vincent Biruta, amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuonekana kuwa huenda Ziwa hilo lina utajiri wa mafuta.
Nchi hizo mbili zimekubaliana kuunda Kamati ya pamoja ya watalaam kuthathmini uwezekano huo wa baadaye kutoa ripoti kwa mataifa hayo.
Uhusiano kati ya Rwanda na DRC kwa muda mrefu umekuwa wenye mashaka kwa sababu za kiusalama lakini mwezi Agosti mwaka 2016, mambo yalionekana kubadilika baada ya rais Kabila na Kagame kukutana baada ya kutofanya hivyo kwa muda mrefu.
Watalaam wanasema kuwa ikiwa mafuta haya yatapatikana na kuanza kuzalishwa, yatakuwa ya manufaa makubwa kiuchumi kwa mataifa hayo jirani.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda, zimetia saini mkataba wa pamoja kutafuta ikiwa kuna mafuta katika Ziwa Kivu.