MISRI

Rais Sisi atangaza miezi mitatu ya hali ya hatari baada ya shambulizi la kigaidi

Jamaa ndugu na marafiki wakiomboleza vifo vya watu 40 walioshambuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Misri
Jamaa ndugu na marafiki wakiomboleza vifo vya watu 40 walioshambuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Misri REUTERS/Mohamed Abd El Ghany

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ametangaza hali ya hatari kwa kipindi cha miezi mitatu baada ya kundi la Islamic State kutekeleza mashambulizi mawili  ya kigaidi katika Kanisa la Coptic mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 40.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yalitekelezwa wakati wauamini walipokuwa Kanisa kuadhimisha Jumapii ya mitende.

Mashambulizi haya yameshutumiwa kimataifa huku rais Abdel Fatha Al Sisi akitoa wito kwa jeshi nchini humo kulinda miundo mbinu muhimu nchini humo ili kuzuia mashambulizi ya kigaidi.

Haya ndio mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kufanyika nchini humo katika siku za hivi karibuni.

Taifa hilo limeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya kigaidi baada ya maandamano ya kisiasa mwaka 2011.

Mazishi ya watu waliopoteza maisha yanafanyika siku ya Jumatatu jijini Cairo.

Serikali ya Misri imekuwa ikisema kuwa lengo la mashambulizi haya ni kuwagawa raia wa Misri kwa misingi ya dini.

Kiongozi wa Kanisa Katoloki duniani Papa Francis, amelaani mashambulizi hayo na kutuma risala za ramirambi kwa jamaa ndugu na marafiki walioathirika.

Rais al-Sisi ametaka jeshi kutoa ulinzi kwa maeneo muhimu nchini humo baada ya shambulizi hilo siku ya Jumapili.