NIGER

Jeshi la Niger lawauwa wapiganaji 57 wa Boko Haram

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau akiwa katikati na walinzi wake
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau akiwa katikati na walinzi wake HO / BOKO HARAM AFP / AFP

Jeshi la Niger linasema limewauwa wapiganaji 57 wa Boko Haram Kusini Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasemakuwa wanajeshi 10 walijeruhiwa katika makabiliano hayo makali yaliyotokea Jumapili iliyopita.

Serikali ya Niger inasema inaendelea kuchunguza ikiwa miongoni mwa wapiganaji hao kulikuwepo mmoja wa viongozi wa kundi hilo.

Mataifa ya Afrika Magharibi yameungana kupambana na wanamgambo wa Boko Haram ambao wameendelea kusababisha mashambulizi na mauaji makubwa hasa nchini Nigeria.

Mbali na Niger na Nigeria, mataifa mengine ambayo yanakabiliana na Boko Haram ni pamoja na Cameroo na Chad.

Kutokana na ongezeko la mashambulizi haya, Niger imetangaza hali ya hatari katika eneo la Diffa, linalowapa hifadhi wakimbizi zaidi ya 300,000 wa nchi hiyo.

Kundi hili ambalo lilianzishwa mwaka 2002 katika jimbo la Maiduguri nchini Nigeria, limetekeleza mauaji ya maelfu ya watu na kuwateka wengine wakiwemo wanafunzi wa Shule ya msingi ya Chibok.

Inaaminiwa kuwa kwa sasa wapiganaji hao wamejificha katika msitu wa Sambisa katika jimbo la Borno.