UN-SUDAN KUSINI

UN yaonya kutokea vifo vya maelfu ya watu kutokana na baa la njaa Afrika

Rais wa Sudan Kusini wakisubiri msaada wa chakula
Rais wa Sudan Kusini wakisubiri msaada wa chakula Wikipedia

Umoja wa Mataifa unaona kuwa maelfu ya watu watapoteza maisha kwa sababu ya baa la njaa katika mataifa yaliyo katika pembe ya bara la Afrika, Yemen na Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Tume hiyo inayoshughulikia wakimbizi katika Umoja huo Adrian Edwards amesema hali hii itatokea kwa sababu ya hali ya ukame inayoshuhudiwa.

Hali hii imesababishwa na kutokuwepo kwa mvua za kutosha katika mataifa hayo lakini pia mizozo isiyoisha.

Mataifa ya Sudan Kusini, Somalia, Yemen na Nigeria ndio yanayokabiliwa zaidi na hali hii kutokana na mapigano yanayoendelea.

Maelfu ya watu wameyakimbia makwao na kuachana na shughuli za kuwasaidia kuinuka kiuchumi.

Umoja wa Mataifa unasema unahitaji Dola za Marekani Bilioni 4.4 kusaidia kukabiliana na hali katika mataifa hayo.

Hadi sasa Umoja huo umefanikiwa kupata Dola za Marekani Milioni 984 sawa na asilimia 21 ya fedha zinazohitajika.

Umoja wa Mataifa unasema, watu 100,000 wanakabiliwa na baa la njaa na wanahitaji msaada wa haraka.

Rais Salva Kiir ameomba jumuiya ya kimataifa kuwasaidia raia wake kupata chakula.