SUDAN KUSINI

Watu 16 wauawa nchini Sudan Kusini katika mapigano kati ya wanajeshi na waasi

Walinda amani wa umoja wa Mataifa walioko mjini Juba, UNMISS, wakionekana kwenye picha wakati fulani walipotekeleza zoezi la kunyang'anya silaha mjni Juba, sasa wanakosolewa kushindwa kuwalinda raia
Walinda amani wa umoja wa Mataifa walioko mjini Juba, UNMISS, wakionekana kwenye picha wakati fulani walipotekeleza zoezi la kunyang'anya silaha mjni Juba, sasa wanakosolewa kushindwa kuwalinda raia UN Photo/Eric Kanalstein

Watu 16 wameuawa katika mapigano kati ya wanajeshi wa serikali ya Sudan Kusini na waasi katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Wau.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la kulinda amani nchini humo linasema mapigano hayo yalitokea mwishoni mwa wiki iliyopita na ni mwendelezo wa makabiliano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi.

Sudan Kusini inasema mapigano hayo yalizuka baada ya waasi kuwavamia kambi yao ya jeshi hilo.

Mauaji haya yanajiri siku chache baada ya rais Salva Kiir kusisitiza kuwa kikosi cha kikanda kilichokubaliwa kupelekwa nchini humo lazima kiwe na wanajeshi kutoka nchi za ukanda pekee.

Jeshi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa watu 3,000 wanapewa hifadhi katika Kanisa moja Katoliki, huku wengine 84 wakipewa hifadhi katika kambi ya Umoja huo.

Serikali ya Juba na waasi wanaongozwa na aliyekuwa Makamu wa rais Salva Kiir, wamekuwa wakihimizwa na Jumuiya ya Kimataifa kutangaza usitishwaji wa mapigano na kuja katika meza ya mazungumzo ya kitaifa.

Viongozi wa nchi hiyo wameshindwa kutekeleza mkata wa kisiasa waliotia saini mwaka 2015 jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.