SOMALIA-UN

UN yasema kipindupindu kimesababisha vifo vya watu 500 nchini Somalia tangu Januari

Wagonjwa waliolazwa nchini Somalia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu
Wagonjwa waliolazwa nchini Somalia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu REUTERS/Andres Martinez Casares

Umoja wa Mataifa unasema kuwa ugonjwa wa kipindupindu umesababisha vifo vya watu 500 nchini Somalia tangu mwezi Januari mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na mauaji hayo, watu wengine zaidi ya 25,000 wameendelea kuathiriwa na ugonjwa huu hatari.

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa, ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kudhibiti ugonjwa huu, huenda idadi ya vifo na watu watakaoathirika ikaongezeka zaidi kufikia mwezi Juni.

Jens Laerke msemaji wa Shirika la Umoja huo linalotoa misaada ya kibinadamu OCHA, amesema maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni majimbo ya Juba na Bakool.

Hili ni janga jipya kwa taifa hilo la pembe ya Afrika ambalo pia linakabiliwa na baa la njaa, ambapo watu Milioni 12 wameendelea kuhangaika.

Hali hii ambayo imesababishwa na ukame kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, imesababisha zaidi ya watu 500,000 kuyakimbia makwao.