CAMEROON-RFI-VYMBO VYA HABARI

Kesi ya Ahmed Abba yaahirishwa, uamuzi kutolewa Jumatatu

Mwandishi wa habari wa RFI katika idhaa ya Hausa nchini Cameroon, Ahmed Abba.
Mwandishi wa habari wa RFI katika idhaa ya Hausa nchini Cameroon, Ahmed Abba. via facebook profile

Mwandishi wa habari wa RFI katika Idhaa ya Hausa nchini Cameroon, Ahmed Abba anakabiliwa na kifungo cha maisha jela. Mahakama ya kijeshi ilimkuta na hatia ya kushindwa kukemea ugaidi na kunufaika na vitendo vya kigaidi. Katika taarifa yake, Uongozi wa RFI una matumaini ya mwandishi wake kuachiwa huru.

Matangazo ya kibiashara

Ahmed Abba alifutiwa kosa la kutetea ugaidi. Kutokana na nakala ya kazi iliyotolewa na RFI ambayo inaonyesha kuwa kinyume na yale upande wa mashtaka ulivyoeleza, Ahmed Abba hakutumia radio kwa kufanya propaganda ya Boko Haram.

Majaji hata hivyo waliona kuwa mwandishi wa habari wa RFI katika Idhaa ya Hausa ana hatia ya kushindwa kutoa taarifa na kunufaika na vitendo vya kigaidi. Kosa hili lina uzito mkubwa. Sheria inatoa kifungo cha maisha kwa kosa hilo. Adhabu hii iliombwa na mwendesha mashtaka. Lakini wanasheria wa Ahmed Abba wanasema kwamba hakuna ushahidi dhidi Ahmed Abba, hakuna vielelezo vinavyoonyesha kuhusika kwa mteja wao.

Tangu mwanzo wa kesi hii, waliomba mteja wao aachiwe huru mara moja. Majaji wanatazamiwa kutoa uamuzi wao Jumatatu ijayo.

Tangazo la RFI

Katika taarifa yake, uongozi wa RFI wamesema wana matumaini kuwa Ahmed Abba ataachiwa huru baada ya uamuzi wa mwisho.

"Wakati wa kesi yake iliposikilizwa siku ya Alhamisi, April 20 mbele ya mahakama ya kijeshi mjini Yaoundé, Ahmed Abba, mwandishi wa habari wa RFI katika idhaa ya Hausa nchini Cameroon, alionekana hana hatia ya kutetea ugaidi, " uongozi wa RFI wamesema.