DRC-SADC-SIASA

SADC kujaribu kupatanisha pande husika katika mgogoro wa DRC

Maaskofu wa Kanisa Katolika ambao wamekua wakiendesha mazungumzo kati ya serikali ya DRC na upinzani Desemba 21, 2016,  Kinshasa.
Maaskofu wa Kanisa Katolika ambao wamekua wakiendesha mazungumzo kati ya serikali ya DRC na upinzani Desemba 21, 2016, Kinshasa. REUTERS/Thomas Mukoya

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imeanza upatanishi kati ya pande husika katika mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano ya Saint-Sylvestre na utekelezaji wake ni moja ya vipengele muhimu vitakavyogubika mazungumzo hayo.

Jaribio hili jipya la kutaka kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini DRC linakuja baada ya rais Joseph Kabila kumteua waziri mkuu.

Ujumbe wa SADC ambako uko ziarani mjini Kinshasa tangu siku ya Jumanne, unakutana na wadau wote katika mgogoro wa Congo kwa lengo la kukusanya maoni na mapendekezo ya serikali na upinzani kwa kutatua mgogoro huo unaoendelea.

Siku ya Alhamisi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Augustine Mahiga, anayeongoza ujumbe wa SADC amewapokea katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa, wajumbe wa chama tawala cha PPRD na washirika wake na kisha muungano wa upinzani wa Rassemblement unaoendelea kugawanyika kuhusu uteuzi wa waziri mkuu mpya.