CAMEROON-RFI-VYMBO VYA HABARI

Ahmed Abba ahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela

Mwandishi wa habari wa RFI katika idhaa ya Hausa nchini Cameroon, Ahmed Abba.
Mwandishi wa habari wa RFI katika idhaa ya Hausa nchini Cameroon, Ahmed Abba. via facebook profile

Nchini Cameroon, mahakama ya kijehi ya Yaounde imemuhukumu kifungo cha miaka 10 jela mwandishi wa habari wa Idhaa ya Hausa ya RFI nchini humo. Mawakili wa Ahmed Aba ambao wanasema mteja wao hana hatia tayari wametangaza kwamba watakata rufaa.

Matangazo ya kibiashara

Ahmed Abba alikamatwa katika mji wa Maroua kaskazini mwa Cameroon Julai 30, 2015. Anatuhumiwa "kula njama katika vitendo vya kigaidi" na "kutotoa taarifa", katika taarifa zake kuhusu mashambulizi ya kundi la Boko Haram.

Julai 30, kwenye muda wa saa nane mchana, gari moja ya polisi iliegesha mbele ya ofisi ya manispaa ya jiji la Maroua. Kama waandishi wengine, Ahmed Abba, mwenye umri wa miaka 39, alikuja kuhudhuria mkutano wa usalama uliyoandaliwa na gavana wa mkoa, siku 8 baada ya mashambulizi mawili yaliyoukumba mji huo.

Muda mchache baadaye askari polisi walimuomba mwandishi wa habari wa Idhaa ya Hausa ya RFI katika mji wa Maroua kuwafuata. Kukamatwa kwake kulifanyika "bila upinzani wowote tena kwa upole," alisema shahidi wa tukio hilo. Ahmed Abba aliwekwa chini ya ulinzi kwa muda wa siku 15, kisha alihamishiwa kwenye makao makuu ya Idara ya upelelezi mjini Yaounde ambapo alikua akizuiliwa. awali shahidi hyo alisema "hakuna mtu anayeweza kumuona, wala familia yake, wala mwanasheria wake, wala daktari, wakati ambapo alipowekwa jela alipigwa. Inabidi kusubiri miezi mitatu ili kupata taarifa zake". "Ahmed Abba yuko salama," Waziri wa Mawasiliano, Issa Bakary Tchiroma aliiambia RFI tarehe 30 Oktoba.

Tarehe 13 Novemba 2015, Ahmed Abba alihojiwa na wapelelezi kutoka Polisi. Wakati huo ndipo alipojua kwamba anashitakiwa kwa "kula njama katika vitendo vya kigaidi" na "kutotoa taarifa". anatuhumiwa kuwa aliwasiliana na wajumbe wa kundi la Boko Haram na kwamba hakuitaarifu serikali kwa yale aliyokusanya kama habari. Alihamishiwa kwenda gereza la mjini Yaounde. Bila uchunguzi wowote, Ofisi ya mashitaka iliiomba mahakama ya kijeshi kushughulikia kesi hiyo.

Kesi hiyo ilianza Februari 29, 2016. Kesi hii ilisikilizwa kwa muda wa miezi saba, ambapo mwanasheria wa Ahmed Abba aliomba mahakama kumuachia huru kwa dhamna, lakini maombi hayo yalikataliwa.

Hakuna ushahidi, hakuna mashahidi

Ahmed Abba alisikilizwa zaidi ya mara 4. Mahakama haijaweka wazi ushahidi wake, wala kusema kuwa ina mashahidi. Wanasheria wake wameendelea kusema kuwa faili ya kesi hiyo iko tupu.