SUDAN KUSINI-UN-USALAMA

Umoja wa Mataifa waitishia kuichukulia vikwazo vipya Sudan Kusini

Mkimbizi akiandamana na askari wa kulinda amani, karibu na kambi ya kulinda raia (POC) ya Umoja wa Mataifa mjini Juba, Oktoba 4, 2016.
Mkimbizi akiandamana na askari wa kulinda amani, karibu na kambi ya kulinda raia (POC) ya Umoja wa Mataifa mjini Juba, Oktoba 4, 2016. ALBERT GONZALEZ FARRAN / AFP

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitishia Sudan Kusini kuichukulia vikwazo vipya kama usitishwaji mapigano hautoheshimishwa. Baadhi ya wanadiplomasia wameonya kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

David Shearer, mwakilishi mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, ameonya wanadiplomasia kwa hali mbaya ya usalama katika wiki za hivi karibuni, kuhu njaa na vurugu kwa misingi ya kikabila vikiendelea kuripotiwa.

Sudan Kusini bado ni taifa changa duniani, na ni chi ambayo inakabiliwa na visa vibaya vya mauaji ambapo katika miezi ya hivi karibuni wafanyakazi 10 wa mashirika ya misaada waliuawa. Vurugu zimeendelea kuongezeka ikiwa imekaribia msimu wa mvua, alionya David Shearer, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu ambaye amebaini kwamba mchakato wa kisiasa ni tete ikilinganishwa na siku za nyuma. "Machafuko yamezidi kuwa mabaya zaidi katika wiki za hivi karibuni".

Waathirika wa kwanza ni raia wa Sudan Kusini ambao ni zaidi ya milioni 5 wanaohitajihaja misaada ya dharura ya kibinadamu kutokana na njaa. Hali ngumu kwa nujimbu wa Mwakilishi wa Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, ambaye pia amebaini kwamba Washington ina wasiwasi kwa yale yanayotokea katika taifa ambalo ilisaidia kuunda. "Ninatoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzingatia hali hii na kutumia uwezo wake, hasa vikwazo vipya na vikwazo vya silaha, vinginevyo vurugu na mauaji vitaendelea kushuhudiwa. Ni lazima kuwa na ishara kwamba maendeleo yanawezekana, "

Mauaji yanafanywa kwa misingi ya kikabila ingawa wanadiplomasia na David Shearer wamekataa kuzungumzia kwa sasa mauaji ya kimbari.