DRC-UN-USALAMA

UN yaonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu katika mji wa Kasai, DRC

Mji wa Kananga katika mkoa wa Kasai ya Kati unakabiliwa na mapigano kati ya wanamgambo wa Kamuina Nsapu na vikosi vya usalama.
Mji wa Kananga katika mkoa wa Kasai ya Kati unakabiliwa na mapigano kati ya wanamgambo wa Kamuina Nsapu na vikosi vya usalama. Junior D. Kannah / AFP

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea kushuhudiwa katika mji wa Kasai, katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Zaidi ya watu 700 000 wako katika hatari katika eneo hilo la Kasai.

Matangazo ya kibiashara

Watu hawa wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu. Afisa wa kuratibu masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC ametoa witowa kutolewa kwa fedha za dharura.

Takriban milioni Dola 75 dola kiasi cha fedha zinazohitajika ili kukabiliana na hali hii mbaya ya kibinadamu katika mji wa Kasai. Kwa mujibu wa Mamadou Diallo, Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, fedha hizi zitatumika ili kukabilia na mahitaji ya dharura kwa watu zaidi ya 730 000 kwa kipindi cha miezi sita ijayo. Watu hao ni waathirika wa machafuko mabaya mauti kati ya wanamgambo wa Kamuina Nsapu na vikosi vya usalama.

Wanawake na watoto ni miongoni mwa watu wanaohitaji maji safi ya kunywa, chakula, na huduma za afya. Kwa mujibu wa afisa wa masuala ya Kibinadamu, ni fedha hizo zinazohitajika ili kukabilian an hali hiyo.