CHAD-SENEGAL-HABRE-HAKI

Mahakama ya Rufaa yathibitisha kifungo cha maisha kwa Hissene Habre

Julai 20, siku ya kwanza ya kesi ya aliyekuwa Rais wa Chad Hissène Habre aondolewe kwa nguvu kutoka mahakamani.
Julai 20, siku ya kwanza ya kesi ya aliyekuwa Rais wa Chad Hissène Habre aondolewe kwa nguvu kutoka mahakamani. AFP PHOTO / SEYLLOU

Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre, ambaye tayari alihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2016, amethibitishiwa kifungo chake siku ya Alhamisi Aprili 27 mbele ya Mahakama maalumu ya Afrika mjini Dakar. Hissene Habre amehukumiwa kifungo cha maisha kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kusalia kimya katika mahakama ya mwanzo, Hissene Habre wakuripoti mahakamani wakati mahakama ilitoa uamuzi wake. Jaji Wafi Ougadèye aliamua kwamba uwepo wake haukua muhimu. kwa hiyo Mahakama ya Rufaa imezingatia uamuzi uliyotolewa na mahakama ya mwanzo. Hissene Habre alipatikana na hatia ya uhalofu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mateso. Hata hivyo, Mahakama ya Rufaa ilifuta uhalifu mwingine wa ubakaji. Upande wa mashitaka umeelezea furaha yao kufuatia uamuzi huo.

Hissene Habre hajawahi kuimtambua mahakam hii maalumu iliyowekwa nchini Senegal na Mahakama ya Kimataifa mwaka 2012. Wanasheria wake walilalamika mara kadahaa wakisema kuwa kesi hiyo iligubikwa na makosa mengi na waliomba mteja wao aachiliwe huru. Itafahamika kwamba Hissene Habre alisalia kimya mara mbili wakati kesi yake ilipokua ikisikilizwa na kukataa kuripoti mahakamani.

Hukumu ya kifungo cha maisha jela imehitimisha mchakato huu wa muda mrefu wa mahakama. Katika hiistoria, itafahamika kwamba kwa mara ya kwanza kiongozi wa zamani wa taifa la Afrika alipatikana na hatia na mahakama maalum ya Afrika na kuhukumiwa katika moja ya nchi za Afrika.