MISRI-VATICAN-DINI-USHIRIKIANO

Papa Francis aelekea Misri kutetea amani na mazungumzo na Waislamu

Le pape François azuru Misri kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidini na ulimwengu wa Kiislamu.
Le pape François azuru Misri kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidini na ulimwengu wa Kiislamu. REUTERS/Alessandro Bianchi

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis anatarajiwa Ijumaa hii, Aprili 28 katika mji wa Misri, Cairo kwa ziara fupi ya siku moja na nusu, ambapo kiongozi hyo anatazamiwa kurejea Roma Jumamosi mchana.

Matangazo ya kibiashara

Lengo la ziara hii ni kutetea amani na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini ya Uislamu wiki tatu baada ya mashambulizi mawili April 9 dhidi Wakristo wa kanisa la Coptic wakati wa maadhimisho ya Jumapili ya matawi, mashambulizi ambayo yaligharimu maisha ya watu 44.

Ziara hiyo inajiri wakati ambapo kuna ongezeko la mauaji ya Wakristo waliopo katika mashariki ya kati hususan wale wa jamii ya kanisa la Coptic.

Mapema mwezi huu kundi la Islamic state lilikiri kutekeleza shambulio la mabomu ya makanisa mawili ya Coptic.

Papa Francis anazuru Misri kwa mwaliko wa rais wa Mirsi Abdel Fattah al-Sisi na Imam Mkuu wa Msikiti wa Al-Azhar Ahmed al-Tayyeb. Papa atakutana na viongozi hao kwa faragha kabla ya kutoa hotuba mbele ya watu wanaoshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Amani, uliyoandaliwa na chuo kikuu cha kifahari cha Al-Azhar.

Ziara hii ya Papa Francis inalenga kuimarisha uhusiano wa kidini na ulimwengu wa Kiislamu.

Papa Francis atakutana na rais wa Misri na atakutana na rais wa taifa hilo ili kutoa hotuba kuhusu amani katika chuo kikuu cha Al-Azhar, taasisi ya masomo ya Kiislamu miongoni mwa madheheu ya Sunni.

Papa Francis ataonyesha umoja wake na mwenzake wa kanisa hilo Tawadrod II akijumuika naye katika kanisa lililoshambuliwa mnamo mwezi Disemba.

Jumamosi asubuhi, wakati wa misa itakayoendeshwa chini ya ulinzi mkali, Papa Francis atakutana na jamii ya watu wachache kutoka kanisa katoliki nchini Misri kabla ya kurejea Roma.