MALI-UFARANSA

Wanajeshi wa Ufaransa wawauawa waasi katika mpaka wa Mali na Burkina Faso

Mwanajeshi wa Ufaransa nchini Mali
Mwanajeshi wa Ufaransa nchini Mali Yutube

Ufaransa inasema wanajeshi wake wamewauawa na kuwakamata zaidi ya waasi 20 katika mpaka wa Mali na Burkina Faso.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi nchini humo linasema kuwa liliwashambulia waasi hao kwa mashambulizi ya angaa lakini haijafahamika walikuwa ni waasi gani.

Hatua hii imekuja baada ya kuuawa kwa mwanajeshi wa Ufaransa katika eneo hilo mwezi Aprili.

Mali imeendelea kukabiliwa na waasi na mwaka 2013, iliomba msaada wa jeshi la Ufaransa ambalo limekuwa likifanya msako na kusaidia mapambana na waasi hao.

Mashambulizi haya yamekuja baada ya bunge la Mali mwishoni mwa wili iliyopita, kupitisha mswada wa kuendelea kuwepo kwa hali ya hatari Kaskazini mwa nchi hiyo kwa sababu za kiusalama.

Ufaransa imetuma wanajeshi wake 4000 kupambana na waasi Kaskazini mwa Mali.