RSF-UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

RSF: Uhuru wa vyombo vya habari uko hatarini

Kiwango cha Uhuru wa habari kimepungua duniani kulingana na ripoti ya mwaka 2017 ya RSF kuhusu suala hilo.
Kiwango cha Uhuru wa habari kimepungua duniani kulingana na ripoti ya mwaka 2017 ya RSF kuhusu suala hilo. Reporters sans Frontières

Wakati ambapo Jumatano hii Mei 3, kunafanyika maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, Shirika la Wanahabari Wasiokuwa na Mpaka (RSF) katika ripoti yake ya hivi karibuni lilitangaza kuwa "Uhuru wa vyombo vya habari uko hatarini katika nchi mbalimbali na zile ambapo demokrasia imeendelea kushamiri.

Matangazo ya kibiashara

RSF inasema kwamba wakati wa maandamano kama katika maeneo ya vita, waandishi wa habari katika baadhi ya nchi, wamekua wakichukuliwa kama mahasimu na kulengwa. Kwa siku hii ya leo, Jumatano hii Mei 3 ambapo inaadhimishwa siku ya Uhuru vyombo vya habari duniani, baadhi ya waandishi wa habari wamefungwa, wengine wamezikimbi nchi zao huku wengine wakiuawa. Hali hii inatokea katika nchi zinazotawaliwa na serikali za kiimla hata katika nchi zilizostawi kidemokrasia.

"Ukandamizaji huu utaisha lini? "amejiuliza katibu mkuu wa Shirika la Wanahabari Wasiokuwa na Mipaka, Christophe Deloire.
Kwa mujibu wa RSF, hali inatisha:" Katika muda wa miaka mitano, waandishi wa habari wameendelea kutishiwa usalama wao, huku kiwango cha uhuru wa vyombo vya habari kikishuka kwa %14 . Karibu theluthi mbili ya nchi zilizoorodheshwa kulishuhudiwa hali mbaya, kwa mujibu wa RSF

Nchi tatu mpya hatimaye zimewekwa katika orodha ya nchi zinazokandamiza uhuru wa vyombo vya habari na katika nchi hizo hali inazidi kuwa mbaya.Nchi hizo ni Burundi, Misri na Bahrain.

RSF inamshtumu rais wa Burundi Pierre Nkurunziza "kufanya ukandamizaji mwaka 2015 dhidi ya vyombo vya habari ambavyo vilirusha hewani habari kuhusu jaribio la mapinduzi baada ya uamuzi wake wa kuwania muhula wa tatu.

RSF inasikitishwa kwamba idadi kubwa ya waandishi wa habari walilazimika kukimbia nchi yao. Kwa mujibu wa RSF, Misri na Bahrain zimekua ni "magereza ya waandishi wa habari" ambapo vyombo vya dola vinatumiwa kwa kukandamiza uhuru wa wa kupata na kutoa habari.