SOMALIA-USALAMA

Waziri wa Ujenzi wa Umma wa Somalia auawa mjini Mogadishu

Uharibifu unaofanywa na kundi la Al shaba Mogadishu.
Uharibifu unaofanywa na kundi la Al shaba Mogadishu. Mohamed ABDIWAHAB / AFP

Waziri wa Ujenzi wa Umma wa Somalia, Abdullahi Siraji, inaonekana kuwa aliuawa kwa ajali, kwa mujibu wa vyanzo vya polisi na serikali vikinukuliwa na shirika la habari la AFP. Gari ambayo alikuwemo Waziri wa Ujenzi wa Umma wa Somalia ilishambuliwa kimakosa na walinzi wa usalama ambao walikuwa nje ya ikulu ya Mogadishu. Katika taarifa yake, serikali imesema "imehuzunika sana na kifo hicho".

Matangazo ya kibiashara

Waziri Siraji, aliye na umri mdogo katika serikali ya Somalia aliuawa alipokuwa katika gari lake. Kwa mujibu wa polisi na vyanzo vya serikali, risasi zilipigwa kimakosa. Kikosi cha ulinzi wa kitaifa walidhani kuwa ni wanamgambo wa Kiislam wa kundi la Al-Shabab.

Vyombo vya habari nchini Somalia, hata hivyo, vimearifu kuwa wahusika wa mauaji wamekamatwa.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, ambaye kwa sasa anazuru Ethiopia, ametangaza kwamba atafupisha ziara yake na kureje nyumbani kuomboleza na wananchi wake na kushiriki katika mazishi ya Waziri Abass." Pia ameahadi kwamba uchunguzi utafanyika na wahusika watahojiwa na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Usalama bado ni moja ya changamoto zinzohitajika kushughilikiwa haraka nchini Somalia, nchi ambayo inaendelea kukumbwa na machafuko yanayosababishwa na kundi la Al Shabab. Kundi hili limeongeza mashambulizi dhidi ngome za jeshi la Somalia na washirika wake ikiwa ni pamoja na kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).

Tangu kuchuku ahatamu ya uongozi wa nchi mwezi Februari, rais Mohamed Abdullahi Mohamed alitangaza vita dhidi ya wapiganaji wa Al Shabab, huku akitoa dola 100,000 kwa mtu yeyote ambaye atatoa taarifa kwa kuzuia mashambulizi.