BURKINA FASO

Kesi dhidi ya Blaise Compaoré yahairishwa tena

Rais wa zamani wa  Burkina Faso, Blaise Compaoré, akiwa ukimbizoni nchini Côté d’Ivoire.
Rais wa zamani wa Burkina Faso, Blaise Compaoré, akiwa ukimbizoni nchini Côté d’Ivoire. © AFP/Issouf Sanogo

Kesi inayomhusisha rais wa zamani wa nchi ya Burkina Faso Blaise Compaoré iliyokuwa imepangwa kuanza  kusikilizwa jana jijini Ouagadougou imeahirishwa tena.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imemkera Wakili wa  kiongozi huyo wa zamani ambaye amesema haelewi ni kwanini kesi hiyo imeahirishwa tena.

Compaore anayeishi nchini Cote Dvoire, na kupewa uraia, anatarajiwa kufunguliwa mashitaka ya mauaji ya wanadamanaji mwaka 2014 katika harakati za kumwondoa  madarakani alipojaribu kubadilisha katiba ili awanie tena urais hata baada ya kuwa madarakani kwa miaka 27.

Chama chake cha  CDP kinaishutumu serikali ambayo kwa sasa inaongozwa na rais Roch Marc Christian Kaboré kuwa na lengo la kulipiza kisasi dhidi ya rais huyo wa zamani na mashtaka hayo ni ya kisiasa.

Tayari kesi dhidi ya Mawaziri 32 wa zamani  imeanza na ikiwa watapatikana na kosa pamoja na rais huyo wa zamani watapewa adhabu ya kifo.

Baadhi ya Mawaziri hao wa zamani walifanikiwa kukimbia nchi hiyo lakini wale waliosalia wamezuiwa kuondoka nchini humo.

Waandamanaji zaidi ya 30 walipoteza maisha katika harakati hizo.