DRC-UNSC

UN yaitaka DRC kutoa ushirikiano kuhusu uchunguzi wa mauaji ya watalaam wake

Mkutano uliopita wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa .
Mkutano uliopita wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa . REUTERS/Shannon Stapleton

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kushirikiana na wachunguzi wake wanaotafiti mauaji ya watalaam wake wawili katika jimbo la Kasai miezi miwili iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa Baraza hilo wameeleza kuwa uchunguzi dhidi ya mauaji ya watalaam hao Michael Sharp, raia wa Marekani na Zaida Catalan, raia wa Sweden utaendelea hadi pale ukweli utakapofahamika.

Aidha, Umoja wa Mataifa umesema kuwa unafuatilia kwa karibu uchunguzi huu wakati huu serikali ya DRC ikiwalaumu waasi wa Kamwina Nsapu, kuhusika na hata kutoa mkanda wa video kuonesha namna mauaji hayo yalivyotekelezwa.

Jimbo la Kasai, limeendelea kushuhudia makabiliano makali kati ya waasi na wanajeshi wa serikali na kusababisha vifo vya watu 400 kati ya mwaka 2015.

Mbali na suala hili, Baraza hilo la Usalama limeitaka serikali ya Kinshasa na upinzani kutekeleza kikamilifu mkataba wa kisiasa uliofikiwa mwaka uliopita.