AFRIKA KUSINI-USALAMA

Mashamba ya wazungu yachomwa moto Afrika Kusini

Chamba la alizeti kaskazini magharibi mwa Afrika Kusini.
Chamba la alizeti kaskazini magharibi mwa Afrika Kusini. Waldo Swiegers/Bloomberg via Getty Images

Nchini Afrika ya Kusini, kumetokea tukio la kibaguzi na kusababisha hasira kwa raia. Mapigano yalitokea siku ya Jumatatu, Mei 8 katika mji mdogo kilomita 200 magharibi mwa Johannesburg baada ya kuachiwa kwa wazungu wawili wanaomiliki mashamba makubwa, ambao wana tuhumiwa kumuua kijana mweusi.

Matangazo ya kibiashara

Kuachiwa kwao kwa dhamana kulizua hali ya sintofahamu na kusababisha hasira kwa wanakijiji ambao walichoma nyumba za wazungu.

Tukio hilo lilitokea wiki mbili zilizopita. Kijana mwenye umri wa miaka 16 aliyetuhumiwa wizi na Wazungu wawili kuwa aliiba alizeti , alifariki baada ya kuanguka kutoka katika gari yao. Wakulima hao wazungu wanasema kuwa kijana huyo alijiua mwenyewe wakati alipokua akijaribu kuruka kutoka katika gari, wakati walikuwa njiani wakielekea katika cha polisi. Lakini shahidi mmoja anasema wakulima wawili wa kizungu walimsukuma kijana huyo kwa makusudi kutoka katika gari yao.

Kesi iko mbele ya mahakama. Siku ya Jumatatu, Wazungu hao wawili wanaotuhumiwa mauaji, waliachiwa kwa dhamana. Taarifa hii ilisababisha mara moja wanakijiji kupandwa na hasira na kuanza kuchoma moto nyumba za wazungu. Kwa uchache nyumba nne zilichomwa moto.

Familia ya kijana huyo aliyefariki wamesema kitendo hicho ni cha ubaguzi wa rangi.

Mwaka jana tayari, wakulima wawili wazungu walikamatwa kwa kosa la kumuweka kijana mmoja mweusi katika jeneza wakimshtumu wizi.