UFARANSA-CHAD-SUDAN-USHIRIKIANO

Mateka wa Ufaransa aliyeachiwa huru awasili N'djamena

Thierry Frezier akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Khartoum, Sudan, 7 Mei 2017.
Thierry Frezier akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Khartoum, Sudan, 7 Mei 2017. AFP/Ashraf Shazly

Mateka wa Ufaransa aliyetekwa nyara Machi 23 mashariki Chad aliwasili siku ya Jumatatu, May 8 katika mji mkuu wa chi hiyo, N'djamena. Thierry Frezier aliachiwa huru nchini Sudan siku ya Jumamosi kabla ya kukabidhiwa viongozi wa Ufaransa mjini N'Djamena.

Matangazo ya kibiashara

Thierry Frezier alisafirishwa na ndege ya sudan hadi N'Djamena, siku Jumatatu, Mei 8, asubuhi. Baada ya dakika chache ya kukutana kwa mazungumzo, Waziri wa Usalama wa Chad, Ahmat Mahamat Bashir, alizungumzia kuhusu masharti yaliyotolewa ili mateka huyo aweze kuachiwa huru.

"Idara zetu zote za usalama, zilishirikiana usiku na mchana mpaka kabla ya siku ya Jumamosi, majambazi walionekana katika kijiji kilio karibu na mji wa Kutum. Bw Frezier aliachiwa huru na hana jeraha hata moja. Wakati huo watekaji nyara wanne walikamatwa na vikosi vya ulinzi vya jamhuri ya Sudan, " alisema Bw Mahamat Bashir.

Katika hali ya kizuizini, Thierry Frezier, mwenye umri wa miaka 60, amesema hakufanyiwa vibaya.

"Hawakua wa kali. Mwanzoni walionekana wakali, lakini baadae mambo yalikuja kuwa sawa. Nimepoteza kilo kumi na mbili lakini hali hiyo ilisababishwa na kazi za usiku, wakati mwingine kutembea, wakati mwingine ngamia, wakati mwingine pikipiki, "Bw Freizer amesema.

Balozi wa Ufaransa nchini Chad, Philippe Lacoste, ambaye alikabidhiwa mateka huyo, aliishukuru serikali ya Chad na Sudan kwa juhudi zilizopelekea kuachiwa huru kwa mateka wa Ufaransa.