DRC-SIASA-USALAMA

Kampeni ya kuwashikiza wanasiasa na viongozi wa DRC kuanza

Rais Joseph Kabila, katika Ikulu ya rais mjini Kinshasa, Jumatano, Aprili 5, 2017, wakati wa hotuba yake kwa taifa.
Rais Joseph Kabila, katika Ikulu ya rais mjini Kinshasa, Jumatano, Aprili 5, 2017, wakati wa hotuba yake kwa taifa. REUTERS/Kenny Katombe

Muungano wa mashirika ya kiraia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo umetangaza kuanza rasmi kampeni ya siku 10 iliyopewa jina “ninaipenda nchi yangu ya DRC” kuomba viongozi wa Serikali kuandaa uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu kama ilivyokubaliwa.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za binadamu barani Afrika la ASADHO nchini humo Jean-Claude Katende, amesema kampeni hiyo ya siku kumi inalenga kuwashinikiza wanasiasa nchini DRC kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika.

Mgogoro wa kisiasa nchini DRC unaendelea kushuhudiwa, baada ya wanasiasa kutoka muungano wa Rassemblement kuhitilafiana.

Hata hivyo usama umeendelea kudorora katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo, hasa katika mkoa wa Kivu ya Kusini, ambapo watu wamekua wakiuawa kila kukicha kwenye barabara inayotoka Bukavu kuelekea Uvira.

Wanaharakati wa mashirika ya kiraia katika mkoa huo wanashtumu viongozi tawala katika mkoa huo kushindwa kudhibiti hali ya usalama.

Wajumbe wa Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katolika nchini DRC, wanaosimamia mazungumzo ya kisiasa nchini humo.
Wajumbe wa Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katolika nchini DRC, wanaosimamia mazungumzo ya kisiasa nchini humo. REUTERS/Thomas Mukoya