ZIMBABWE-MUGABE-SINGAPORE-AFYA

Rais Robert Mugabe kupatiwa matibabu Singapore

Robert Mugabe, katika mkutano wa 34 wa SADC, zambia, Agosti 18 mwaka 2014.
Robert Mugabe, katika mkutano wa 34 wa SADC, zambia, Agosti 18 mwaka 2014. REUTERS/Philimon Bulawayo

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amekwenda nchini Singapore kuonana na madaktari wake. Rais Robert Mugabe anatarajiwa kurejea nyumbani mwishoni mwa wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Gazeti la serikali la The Herald limeripoti kuwa rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93, alikwenda nchini Singapore siku ya Jumatatu kuonana na madaktari wake kama ilivyo ada.

Hata hivyo Gazeti hilo limeripoti kuwa rais Mugabe anatarajiwa kurejea nyumbani mwishoni mwa wiki hii.

Tangu kuingia madarkani mwaka 1980, Mugabe ambaye ametangaza kuwania tena urais mwakani ujao licha ya kuwa na umri mkubwa, ameskuwa akienda kuangalia afya yake na kupumzika Singapore tangu, na mara ya mwisho ilikuwa ni mwezi Machi.

Mugabe amekuwa akitembea kwa shida na kusinzia katika mikutano mbalimbali kama ilivyoshuhudiwa hivi karibuni katika mkutano wa Kimataufa wa uchumi kwa bara laAfrika uliofanyika nchini Afrika Kusini.

Wapinzani wamekuwa wakijaribu kumshinikiza rais Mugabe ajiuzulu na kuachana na siasa kwa sababu ya umri na afya yake bila mafanikio.