DRC-UDPS-TSHISEKEDI-HAKI

UDPS yailaumu serikali ya DRC kushindwa kusafirisha mwili wa Tshisekedi

Wafuasi wa Etienne Tshisekedi nje ya makao makuu ya chama cha UDPS katika mjiwa wa Kinshasa, Oktoba 27, 2016.
Wafuasi wa Etienne Tshisekedi nje ya makao makuu ya chama cha UDPS katika mjiwa wa Kinshasa, Oktoba 27, 2016. RFI/Sonia Rolley

Chama kikuu cha upinzani cha UDPS cha nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kimeishutumu serikali ya Kinshasa kwa kuchukua hatua inayozuia mashirika ya ndege kuusafirisha mwili wa kinara wa upinzani Etienne Tshisekedi.

Matangazo ya kibiashara

Etienne Tshisekedi aliyeaga dunia mwanzoni mwa mwezi February mwaka huu kutoka Brussels na kuurejesha nyumbani hadi Kinshasa.

Afisa wa mwasiliano wa chama hicho Augustin Kabuya amesema kuwa chama hicho kimepanga kuurejesha nyumbani mwili wa aliyekuwa kinara wa upinzani Etienne Tshisekedi Mei 12 mwaka huu, na kwamba tangazo la serikali kuzuia makampuni ya usafirishaji wa ndege limekuja wakati kukiwa na hali ya wasiwasi baada ya Ofisi ya Polisi iliyojirani na chama hicho Kuchomwa moto na watu wasiojulikana.

Kabuya amesema kuwa idaidi kubwa ya Polisi wamepelekwa katika maeneo jirani ya Ofisi za Chama hicho na kwamba kumekuwa hali ya sintofahamu.