COTE D'IVOIRE-USALAMA

Hali ya sintofahamu yaendelea kushuhudiwa Bouaké

Askari wakikosi cha  ulinzi wa rais wakizingira kambi ya askari walioasi, Mei 12, 2017, Abidjan.
Askari wakikosi cha ulinzi wa rais wakizingira kambi ya askari walioasi, Mei 12, 2017, Abidjan. REUTERS/Luc Gnago

Nchini Cote d'Ivoire, kulitokea machafuko asubuhi ya Jumapili, Mei 14, katika mji wa Bouake, katikati mwa nchi hiyo. Mji huo, tangu Ijumaa, umeku ni kitovu cha uasi wa askari wanaodai malipo ya malimbikzo. Wakazi ambao walikusanyika wakipinga askari waasi walipigwa vibaya. Mpaka inaarifiwa kuwa mtu mmoja amepoteza maisha.

Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa saa 6:30, Jumapili asubuhi katika eneo la kituo cha mabasi katika mji wa Bouake, ambapo watu walikusanyika ili kuandaa maandamano dhidi ya askari waasi. Muda mchache baadae, magari mawili yaliokua yamejaa askari waliojihami kwa silaha za kivita walianza kurusha risasi hewani na kwenye umati wa watu," amesema shahidi.

Inaarifiwa kuwa watu wanane walijeruhiwa papo hapo, ambapo wawili walijeruhiwa kwa risasi. Wengine walipigwa na askari walioasi. Madaktari katika hospitali hiyo, pia wanatibu majeraha ya risasi na wengine kuvunjika miguu na mikono.

Askari waasi na serikali wameendelea, kila upande kuonyesha msimamo wake kwa muda wa siku mbili sasa, tangu siku ya Jumamosi.

Raia wameelezea wasiwasi wao kuhusu hali hiyo wakise akwamba wao ndio walengwa wa kwanza katika ghasia hizo, kama Jumamosi asubuhi katika mji wa Bouaké.

"Wao [waasi] wanaweza kurusha risasi hewani, mtu anaweza kuelewa lakini kurusha risasi kwenye umati wa watu, hali hiyo inatutia wasiwasi, " amesema mkazi mmoja wa Bouaké.

Waasi hao wa zamani wanadai kulipwa Euro 18,000 kwa kile mwanajeshi, lakini wamefanikiwa kulipwa Euro 7,500 na ripoti zinasema kuwa ilikuwa imepangwa kuwa watapokea malipo mengine mwezi huu.

Hata hivyo, baadhi ya wanajeshi walijitokeza baadaye na kudai kuwa hawakushauriwa kuhusu hatua iliyofikiwa na msemaji wao.

Rais Outtara amekuwa akisema kuwa nchi yake inapitia kipindi kigumu cha kisiasa kwa sababu ya kushuka kwa biashara ya Cocoa.