DRC-MOBUTU-UTAWALA

DRC yaadhimisha miaka 20 ya kuanguka kwa utawala wa Mobutu

Aliekua rais wa Zaire (DRC) Mobutu Sese Seko.
Aliekua rais wa Zaire (DRC) Mobutu Sese Seko. (Photo : AFP)

Utawala wa aliyekuwa rais wa DRC (Zaire wakati huo) Mobutu Sese Seko ulianguka tarehe 16 Mei 1997. Siku iliyofuata, tarehe 17, vikosi vya wapiganaji wa kundi la waasi la AFDL viliingia kwa ushindi mkubwa katika mji wa Kinshasa, bila ya upinzani wowote kutoka jeshi la Mobutu (FAZ).

Matangazo ya kibiashara

Mei 16, historia inaeleza kuwa Mobutu alikua na hofu ya kuanguka kwa utawala wake. Wakati wote huo Laurent Desire Kabilaalikua tayari aliingia kwa uficho kwa wiki kadhaa katika mji wa Kinshasa, huku askari wake wakipiga kambi kwenye barabara kuu zinazoingia katika mkuu wa nchi hiyo. Baada ya kushindwa kwa mazungumzo chini ya uangalizi wa Nelson Mandela na Omar Bongo, Laurent Kabila alitangaza kuwa utawala wa "Mubutu umekwisha": "Najua kuwa Mobutu sasa amekwisha. Nguvu tena hana. Kwa sasa amezingirwa. "

Kushoto, aliekua rais wa Zaire (DRC) Mobutu Sese Seko Mei 1997. Kilia, Iviart Izamba (DRC), kiti cha Mobutu kilichotengenezwa kwa chuma na ngozi.
Kushoto, aliekua rais wa Zaire (DRC) Mobutu Sese Seko Mei 1997. Kilia, Iviart Izamba (DRC), kiti cha Mobutu kilichotengenezwa kwa chuma na ngozi. WALTER DHLADHLA (AFP)/JO VAN DE VYVER, MRAC TERVUREN

Saa 7:50 asubuhi tarehe 16 Mei 1997, msafara wa Mobutu Sese Seko ulionekana ukielekea katika uwanja wa ndege wa Ndjili. Ndege ya Mobutu Sese Seko ilitua katika katika kijiji alikozaliwa cha Gbadolite. Tarehe 17 vijana wa kabila (kadogo) wakivalia sare fupi za buti nyeusi za plastiki waliingia katika mji wa Kinshasa kama wakombozi wa taifa la Congo. Kwenye barabara kuu iliyobatizwa Juni 30 , wakaazi wa mji wa Kinshasa waliwalaki vijana hao na kuwapongeza kwa kazi kubwa walioifanya ya kumtimua Mobotu Sese Seko, aliyetawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 ."Mobutu kaondoka, Kabila tayari amewasili. Tupo katika furaha! tuna fuarha ya kukombolewa, " walisem awakaazi hao.

Rais huyo aliyekua akidai kuwa ni kiongozi wa milele wa taifa hilo kubwa la afrika ya Kati alipatwa na maradhi ya saratani kwenye kibofu na kwenye uti wa mgongo. François Joseph Mobutu Nzanga, mwanawe mkubwa,alimshauri, kuondoka nchini. "Baba," kama alivyokua akiitwa na wananchi wa Zaire wakati huo, aliona kuwa ndoto zake mbili zimezima ikiwa ni pamoja na kufariki akiwa rais na kufariki akiwa ndani ya nchi. Mobutu ambaye alikua na umri wa miaka 76 aliondoka nchini akipitia kwenye uwanja wa ndege wa Moanda, karibu na kijiji cha Gbadolite hadi Lome. Mobutu aliendelea hadi Morocco, ambapo kifo kilimkuta.

Joseph Désiré Mobutu aliishi katika mji mkuu wa Morocco, Rabat kwa muda wa miezi 5 kabla ya kufariki kwa maradhi ya saratani. Morocco ilikua mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa Zaire.

Kanali Mobutu Sese Seko, alamaarufue «Chui wa Kinshasa» Septemba 16, 1960. Katibu Dola wa  serikali ya Patrice Lumumba, ambaye aliongoza Novemba 24, 1965 mapinduzi ya kijeshi dhidi Joseph Kasavubu, rais wa kwanza wa DR Congo.
Kanali Mobutu Sese Seko, alamaarufue «Chui wa Kinshasa» Septemba 16, 1960. Katibu Dola wa serikali ya Patrice Lumumba, ambaye aliongoza Novemba 24, 1965 mapinduzi ya kijeshi dhidi Joseph Kasavubu, rais wa kwanza wa DR Congo. AFP