CAR-USALAMA

Askari 6 wa UN na raia 26 wauawa Bangassou

Kikosi cha Umoja wa matiafa ncini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) kikipiga doria katika mji wa Bangui mwaka 2016.
Kikosi cha Umoja wa matiafa ncini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) kikipiga doria katika mji wa Bangui mwaka 2016. ISSOUF SANOGO / AFP

Hali ya utulivu imerejea katika mji wa Bangassou uliokumbwa na machafuko baada ya kuvamiwa na kundi la watu wenye silaha na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30 kwa mujibu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca).

Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa kikosi cha askari wa Umoja wa Matiafa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jenerali Bala Keita, ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali hatari inayoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.

"Kuna vijana ambao wameshindikana kudhibitiwa na wamekua wakitumia hali hiyo kwa kufanya uhalifu dhidi ya wengine, lakini tutafanya kilio chini ya uwezo wetu vijana hao wadhibitiwe ili kuzuia kusitokei ulipizaji kisasi, hali ambayo huenda ikjasababisa vifo vya watu wengi, " amesema Jenerali Bala Keita.

Ni kwa mara ya kwanza tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) kufanya mkutano na waandishi wa habari tangu kuzuka kwa machafuko haya yaliyoukumba mji wa Bangassou siku ya Jumamosi Mei 13.

Watu 7,000 waliyahama makazi yao na kwa sasa wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha, huku wakikabiliwa na ukosefu wa maji safi.

"Tunaomba mapigano yasitishwe mara moja. Pia tunaomba jumuiya ya kimataifa kuongeza jitihada kwa kukomesha hali hii, " amesema Frédéric Manantsoa, mwakilishi wa shirika la kimataifa la Madaktari wasiokuwa na Mipaka (MSF) nchini Jamhuri ya afrika ya Kati.