SUDAN-SAUDI RABAT

Rais Bashir aalikwa katika mkutano wa nchi za Kiarabu nchini Saudi Arabia, ataonana na Trump

Saudi Arabia imemwalika rais wa Sudan, Omar al-Bashir, anayetakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya ICC katika mkutano wa Kimataifa wa nchi za kiarabu na viongozi wa Kiislamu.

Rais wa Sudan Omar-al Bashir
Rais wa Sudan Omar-al Bashir REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo pia utahudhuriwa na rais wa Marekani Donald Trump, mkutano utakaofanyika siku ya Jumapili.

Hii itakuwa ni ziara ya kwanza nje ya nchi kwa Trump aliyeingia madarakani mwezi Januari.

Ikulu ya White House imesema atawahotubia viongozi wa nchi za kiarabu na viongozi wa Kiislamu kuhusu namna mataifa ya Kiislamu yanavyoweza kupata amani ya kudumu.

Mahakama ya ICC imekuwa ikimtafuta rais Bashir tangu mwaka 2009 kwa makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika jimbo la Darfur, na kusababisha zaidi ya watu 300,000 kupoteza maisha tuhma ambazo amezikataa.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu kama  Amnesty International, Human Rights Watch pamoja na ICC yenyewe wamekuwa wakitoa wito kwa kukamatwa kwa rais Bashir.