LIBYA-USALAMA

Zaidi ya watu 60 wauwawa kusini mwa Libya

Mapigano yaendelea kurindima kusini mwa Libya.
Mapigano yaendelea kurindima kusini mwa Libya. REUTERS/Stringer

Maafisa wa usalama nchini Libya, wanasema kwamba zaidi ya watu 60 wameuwawa, katika mapigano makali kati ya makundi mawili hasimu, Kusini mwa nchi hiyo. Maafisa hao wanasema kua watu wengi wamejeruhiwa katika mapigano hayo.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ambapo msemaji wa kundi la Libyan National Army, ametangaza kwamba uwanja wake wa ndege wa Brak al-Shati, ulivamiwa.

Hata hivyo inasemekana kuwa kundi moja linalojulikana kwa jina la Third Force ndilo lililotekeleza shambulio hilo.

Mapema mwezi huu, kiongozi mkuu wa Libyan National Army, Khalifa Haftar, alikutana na Fayez al-Sarraj, kiongozi mkuu wa serikali iliyoko Tripoli ,ili kujaribu kuzima uhasama unaotokota Kusini mwa nchi hiyo.

Eneo hilo limekuwa linaendelea kukabiliwa na mdororo wa usalama kutokana na taharuki inayotanda kati ya wanaounga mkono serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa iliyoko katika mji mkuu Tripoli, na wapinzani wao.

Libya inaendelea kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu kuangushwa kwa utawala wa hayati Kanali Muammar Gaddaffi Oktoba 20 mwaka 2011.