EU-AFRIKA MASHARIKI

EU kuiondolea Burundi vikwazo ikiwa muafaka wa kisiasa utapatikana

Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza
Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza AFP PHOTO/Carl DE SOUZA

Umoja wa Ulaya EU utaiondolea vikwazo Burundi ikiwa muafaka wa kisiasa utapatikana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vikikoma.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na Idhaa hii Balozi wa EU nchini Tanzania na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Roeland van de Geer, amesema Umoja huo utaindolea vikwazo Burundi mara muafaka wa kisiasa utakapopatikana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kukoma,wala sio kuhusu shinikizo za mkataba wa kibishara kati yake na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika mashariki raisi wa Uganda Yoweri Museven akitamatisha mkutano wa 18 jijini Dar es salaam alipinga umoja wa Ulaya ama kwa makusudi au kutokujua mipaka yake kuingilia masuala ya ndani ya nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki akitolea mfano vikwazo ambavyo imetangaza dhidi ya Burundi.

“Umoja wa Ulaya na wadau wengine hivi karibuni kulikuwa na mazungumzo kuhusu kuiwekea vikwazo Sudan Kusini katika umoja wa Mataifa...hii ni tabia gani mbaya ambayo umoja wa Ulaya mnayo, mimi ndio naijua Sudan Kusini”. Amesema Museveni.

Kuhusu mkataba wa kiuchumi kati ya umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki, rais Museveni amesema nchi hizo haziwezi kuutia saini wakati kuna wanachama wao wengine wanawekewa vikwazo.