Waafrika kusini waandamana kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Imechapishwa:
Mamia ya waandamanaji wamejitokeza katika mitaa ya mjini Pritoria kupinga ongezeko la vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto nchini Afrika kusini ikiwemo kushambuliwa kingono.
Waandamanaji hao Wakiitikia wito uliotolewa na kundi lililojiita sio kwa jina langu, wengi wao wanaume walitembea katika mitaa ya jiji hilo nchini Afrika kusini nyuma ya mwanamke aliyevalia mavazi meupe kuanzia kichwani hadi miguuni.
Hivi karibuni kumeripotiwa mfululizo wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto hatua ambayo raisi wa nchi hiyo Jacob Zuma alitangaza hali hiyo kuwa janga.
Afrika kusini inatajwa kuwa kiwango cha juu cha vitendo vya ukatili wa kingono duniani.
Kwa mujibu wa polisi vitendo elfu 64 vimeripotiwa mwaka jana pekee.