DRC-USALAMA-SIASA

Mauaji Kasai: Mbunge Clément Kanku awekwa mashakani

Mji wa Kananga katika mkoa wa Kasaiya Kati unaendelea kukabiliwa na makabiliano kati ya kundi la Kamuina Nsapu na vikosi vya usalam nchini DRC.
Mji wa Kananga katika mkoa wa Kasaiya Kati unaendelea kukabiliwa na makabiliano kati ya kundi la Kamuina Nsapu na vikosi vya usalam nchini DRC. Junior D. Kannah / AFP

Sauti iliyorekodiwa ambayo inafananishwa na ile ya Mbunge Clément Kanku imezua hali ya sintofahamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kusikika katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo kati ya mbunge wa mkoa wa Kasai, ambaye aliwahi kuwa waziri pamoja na mtu anayedaiwa kuwa mwanamgambo wa Kamuina Nsapu anayemueleza jinsi mashambulizi yaliyokua yakiendelea katika mji wa Kasai yamerushwa katika mitando mbalimbali ya kijamii.

Gazeti la New York Times ndio lilifichua Jumapili Mei 21 uwepo wa sauti hiyo iliorekodiwa ambayo ilikuwa katika kompyuta ya Zaida Catalan, mtaalam wa Umoja wa Mataifa alieuawa mwezi Machi pamoja na mwenzake Michael Sharp.

Inasemekana kuwa sauti hii ilirikodiwa na kuanza kurushwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii Agosti 8, yaani kabla ya kifo cha Kamuina Nsapu na mauaji makubwa mengine ambayo yalifuata.

Hata hivyo, serikali na viongozi wengine walikua wanajua uwepowa faili hizi za za sauti, kwa sababu kwa mujibu wa taarifa zetu, ni mazungumzo au sauti ambazo zilitengenezwa na idara ya ujasu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. siku chache baada ya sauti hizo kurekodiwa, Mbunge Clément Kanku alitakiwa kujieleza mbele ya mashahidi kwa ombi la Waziri wa Mambo ya Ndani Evariste Boshab.

Faili hizi za sauti zina mazungumzo ya aina mbili kupitia njia ya simu kwa lugha ya Thisluba, ambapo anasikika mwanamgambo au mtu anayedaiwa kuwa mwanamgambo wa kamuina Nsapu, akimuelezea mbunge Clément Kanku, vitendo viovu ambavyo alitekeleza. "Tumechoma Tshimbulu" anaeleza mtu huyo anaedaiwa kuwa mwanamgambo wa Kamuina Nsapu. "Ni vizuri kuwa mumefanya jambo hilo," alijibu Clément Kanku katika mazungumzo ya kwanza.

Katika mazungumzo ya pili, wawili hao wanasikika wakizungumzia mauaji ya afisa wa jeshi na walinzi wake. Hata hivyo mbunge Clément Kanku ameomba maelezo ya kina kuhusu kuhusika kwake katika mazungumzo hayo lakini hajakubaliwa. Katika mashambulizi hayo watu 9 waliuawa.

Haijulikani ni maelezo gani mbunge Clément Kanku alitoa kwa serikali lakini hiyo haikukataza mwezi Desemba mwaka jana mbunge huyo kuteuliwa katika serikali ya Sami Badibanga, mpaka alivyojiuzulu. Akihojiwa na RFI, Clément Kanku haijajibu maombi yetu kwa mahojiano.