GAMBIA-JAMMEH-UCHUMI

Mali ya rais wa zamani wa Gambia kuzuiliwa

Aliyekuwa rais wa Gambia, Yahya Jammeh, atuhumiwa kupora Dola milioni 50. (Picha ya zamani).
Aliyekuwa rais wa Gambia, Yahya Jammeh, atuhumiwa kupora Dola milioni 50. (Picha ya zamani). REUTERS/Carlos Garcia Rawlins/Files

Nchini Gambia, kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa mali ya umma kwa upande wa aliyekua rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh, serikali imeanza kufuatilia mali ya kiongozi huyo wa zamani wa Gambia.

Matangazo ya kibiashara

Yahya Jammeh anatuhumiwa kukupora Dola zaidi ya milioni 50 (sawa na Euro zaidi ya milioni 44), kabla ya kukimbilia uhamishoni.

Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, Mei 22, katika mji mkuu wa Gambia, Banjul, Waziri wa Sheria, Aboubacar Tambadou, alitangaza kuzuliwa kwa mali ya aliyekuwa rais wa Gambia Yahya jammeh. Uamuzi wa kumzuia kutumia mali yake ikiwa mahakama itamuagiza kuilipa serikali.

Uchunguzi wa awali wa polisi unataja kiwango cha fedha ambazo Yahya Jammeh alipora. Kwa mujibu wa Wizara ya Sheria, kati ya mwaka 2006 na 2017, Euro zaidi ya milioni 3 nusu zilitoweka kutoka mfuko wa usalama wa kijamii na ufadhili wa makazi.

Mbaya zaidi, katika miaka minne iliyopita, Yahya Jammeh aliagiza kutoa kinyume cha sheria Euro zaidi ya milioni 44 kwenye Benki Kuu, kutoka katika akaunti za shirika la simu la umma, Gamtel.

Mahakama kuu imetoa idhni kwa Wizara ya Sheria kuzuia mali yote inayojulikana kuwa ni ya dikteta wa zamani nchini Gambia. Kwa jumla, zaidi ya mashamba mia moja, akaunti 88 za benki na makampuni 14 ni miongoni mwa mali za kiongozi huyo wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh.