DRC-UFARANSA

Raia wa Ufaransa aliyetekwa nchini DRC aachiliwa huru

Picha ya eneo la Namoya lenye utajiri wa dhahabu nchini DRC
Picha ya eneo la Namoya lenye utajiri wa dhahabu nchini DRC rfi

Raia wa Ufaransa aliyetekwa mwezi Machi mwaka huu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akifanya kazi katika mgodi wa dhahabu, ameachiliwa huru. 

Matangazo ya kibiashara

Mateka huyo ambaye jina lake halijafahamika, alikuwa anafanya kazi katika kampuni ya madini ya Barno katika mkoa wa Maniema inayomilikiwa na wawakezaji kutoka nchini Canada.

Rais Macron amepongeza mamlaka nchini DRC kwa kushughulikia  kuachiliwa huru kwa mateka huyo.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa ilitangaza mwezi Machi kuwa watu waliojihami kwa silaha  waliwateka wafanyakazi wa mgodini wapatao watano akiwemo Mfaransa mmoja, raia wa Tanzania na wengine wa DRC Mashariki mwa nchi hiyo.

Serikali ya DRC kupitia Wizara ya Mambo ya ndani imethibtisha kuachiliwa huru kwa mateka huyo, hatua inayokuja baada ya mateka wanne akiwemo Mtanzania mmoja kuachiliwa huru mwezi Aprili.

Kundi la mai mai mutomboki linadaiwa kutekeleza utekaji huu ambapo kiongozi wa kundi hilo Sheikh Hassan” aliiambia RFI kuwa liliwateka watu hao ili kushinikiza kampuni hiyo ya Benro kutekeleza ahadi zake kwa wenyeji wa eneo hilo kama ujenzi wa barabara.