MOROCCO-USALAMA

Umati wa waandamanaji wamiminika katika mitaa ya mji wa Rabat

Maelfu ya waandamanaji waendelea na maandamano katika mji wa Rabat.
Maelfu ya waandamanaji waendelea na maandamano katika mji wa Rabat. REUTERS

Nchini Morocco, barabara zinazoingia katika mitaa maarufu katika mji mkuu wa nchi hiyo, Rabat, zimefungwa na maelfu ya waandamanaji waliomiminika mitaani. Wakati huo huo maandamano mengine yanaendelea Kaskazini mwa nchi hiyo kwa miezi saba sasa.

Matangazo ya kibiashara

Hali ya wasiwasi iliripotiwa tangu siku ya Ijumaa baada ya vurugu kuzuka nje ya mji wa al-Hoceima ambapo polisi ilijaribu kumshikilia mwanaharakati maarufu Nasser Zefzafi.

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama nchini Morocco, Nasser Zefzafi alivuruga ibada iliyokuwa ikiendelea katika moja ya misikiti katika mji wa Rabat.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Morocoo hali ya wasiwasi ilianza tangu mwezi Oktoba mwaka 2016 kutokana na kisa cha al-Hoceima, mfanyabiashara maarufu wa samaki, aliyeuawa wakati akiwazuia maofisa wa serikali wasiharibu ghala la samaki wake.

Kwa mujibu wa chanzo cha usalma, kiwango cha usalama kimeshuka kabisa tangu kuzuka kwa vurugu hizo.