MOROCCO-USALAMA

Kiongozi wa maandamano nchini Morocco, kuhamishiwa Casablanca

Zefzafi Nasser, kiongozi wa maandamano yanayolikumba jimbo la Rif baada ya kifo cha muuzaji samaki aliyeuawa na maafisa wa usalama, hapa ni wakati wa maandamano ya Mei 18, 2017.
Zefzafi Nasser, kiongozi wa maandamano yanayolikumba jimbo la Rif baada ya kifo cha muuzaji samaki aliyeuawa na maafisa wa usalama, hapa ni wakati wa maandamano ya Mei 18, 2017. REUTERS/Youssef Boudlal

Nchini Morocco, Zefzafi Nasser, kiongozi wa maandamano yanayilikumba jimbo la Rif, alikamatwa siku ya Jumatatu asubuhi Mei 29, baada ya machafuko yaliodumu siku tatu.

Matangazo ya kibiashara

Ijumaa iliyopita, kiongozi huyo wa kundi la "Hirak" alisababisha serikali kuingiliwa na wasiwasi, baada ya kukatiza hotuba ya sala kuu ya siku hiyo katika msikiti wa Al Hoceima, mji mkuu wa mkoa wa Rif, ambapo maandamano yalianza miezi sita iliopita.

Zefzafi Nasser alikamatwa na watu wengine na kisha walihamishwa mara moja katika mji wa Casablanca kwa ajili ya muendelezo wa uchunguzi. Uchunguzi ambao unaendeshwa na na Kati Mahakama kuu ya Polisi. Bw Nasser anajiunga na wanaharakati ishirini ambao tayari wamewekwa chini ya ulinzi na walikamatwa Jumamosi na Jumapili katika mji wa Al Hoceima.

Kwa mujibu wa Ibara ya 221 ya sheria ya jinai, Nasser Zefzafi anakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuvuruga shughuli za kidini. Pia inaaminika kuwa alipata msaada kutoka kwa mashirika ya kigeni, hali ambayo inaweza kuongeza adhabu ya miaka 20 jela kwa kuhatarisha usalama wa taifa.

Tangu Jumapili, hali ya utulivu inaonekana kurudi katika mji wa Al Hoceima, ambapo kulitokea makabiliano makali na maandamano zaidi ya miezi sita iliopita baada ya kifo cha muuzaji samaki kiliozua hali ya sintofahamu nchini Morocco. Waandamanaji wanadai hatua ya kijamii na kiuchumi kwa kurahisishia jimbo hilo la kaskazini-mashariki ya Morocco, lenye wakaazi wengi maskini nchini humo.

Nasser Zefzafi ana ushawishi mkubwa kwa vijana wa Morocco.

Mashirika ya kiraia kama kama vile ATTAC yenye makao yake makuu mjini Casablanca, yanalaani kukamatwa kwa watu hao.