DRC-EBOLA

DRC yasema imefanikiwa kudhibiti maambukizi ya Ebola

Wataalam wa afya wanaopamabana na maambukizi ya Ebola nchini DRC
Wataalam wa afya wanaopamabana na maambukizi ya Ebola nchini DRC cdn.mg

Wizara ya afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema imefanikiwa kudhibiti maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Matangazo ya kibiashara

Hakikisho hili limetolewa na Waziri Oly Ilunga Kalenga jijini Kinshasa, ambaye ameeleza kuwa kwa muda wa siku 21 zilizopita, hakuna maambukizi yoyote mapya yaliyoripotiwa.

“Hadi katika hatua hii, tunaweza kusema kwa uhakika kuwa, tumedhibiti maambukizi haya,”

“Tunawashukuru watalaam wa kitaifa na Kimataifa waliohusika katika jitihada za kudhibiti maambukizi haya,” amesema Waziri Kalenga.

Watu wanne walipoteza maisha baada ya kuambukizwa ugonjwa huu hatari uliozuka katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo tarehe 11 mwezi Mei, karibu na nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Hatua hii inakuja baada ya maafisa wa afya kuidhinisha matumizi ya chanjo mpya kujaribu kupambana na ugonjwa huu hatari.

Imekuwa mara ya nane kwa nchi hiyo yenye utajiri wa misitu kupata maambukizi hayo ambayo yalibainika mara ya kwanza katika taifa hilo karibu na mto Ebola, mwaka 1976.