DRC-MAREKANI-KABILA-USHIRIKIANO

Marekani yamchukulia vikwazo mshirika wa karibu wa Kabila

Kikosi cha kuzima fujo kikipiga doria kabla ya kutawanyika waandamanaji si mbali na jengo la Bunge katika mji wa Kinshasa, Januari 19 mwaka 2015.
Kikosi cha kuzima fujo kikipiga doria kabla ya kutawanyika waandamanaji si mbali na jengo la Bunge katika mji wa Kinshasa, Januari 19 mwaka 2015. RFI/LL.Westerhoff

Siku 3 baada ya Umoja wa Ulaya kutangaza vikwazo dhidi ya maafisa tisa wa serikali ya Jamahuri ya Kidemokrasia ya Congo, Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Afisa mkuu anayesimamia maswala ya kijeshi na mtu wa karibu wa rais Joseph Kabila, jenerali François Olenga.

Matangazo ya kibiashara

Marekani inalituhumu jeshi la ulinzi wa rais, Republican Guard, linaloongozwa na afisa huyo, kwa kunyonga, pia kuweka watu mbaroni bila hatia.

Vikwazo hivyo ni pamoja na kuzuwiwa mali zake zote anaziohifadhi nchini Marekani na kupiga marufuku ushirikiano wake na makampuni binafsi nchini Marekani.

Itakufamika kwamba serikali na vyama vunavyoiunga mkono wameendelea kushtumu Umoja wa Ulaya kuingilia uhuru wa taifa la DR Congo.

Visa vya mauaji na visa vingine vinavyokiuka haki za binadamu vinaendelea kushuhudiwa nchini DRC, huku vyomvo vya usalama na ulinzi vikinyooshewa kidole cha lawama.