Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Rais wa DRC Joseph Kabila atembelea mji wa Kananga, reli ya kisasa yazinduliwa nchini Kenya, Marekani yajiondoa mkataba wa Paris

Sauti 21:16
Ofisi kuu ya shirika la Unicef mjini Kananga, DRC, ikiwa chini ya ulinzi wa kikosi cha UN kutoka Uruguay
Ofisi kuu ya shirika la Unicef mjini Kananga, DRC, ikiwa chini ya ulinzi wa kikosi cha UN kutoka Uruguay RFI/Sonia Rolley

Katika makala hii tumeangazia kuzinduliwa kwa reli ya kisasa na treni ya mwendo kasi inayounganisha miji ya Nairobi na Mombasa ambapo rais Uhuru Kenyatta amesema ambao wataharibu miundo mbinu hiyo watapewa adhabu ya kunyongwa, ziara ya rais wa DRC Joseph kabila kwenye mji wa Kasai ambako yalishuhudiwa mauaji makubwa, tumegusia habari za ukanda wa afrika mashariki na pia hatua ya Marekani kujiondoa katika mkataba wa Paris kuhusu mazingira, na mabadiliko ya tabia nchi.