ECOWAS-USHIRIKIANO

Faure Gnassingbé achaguliwa kuwa rais wa ECOWAS

Rais wa Togo Faure Gnassingbé ambaye amechaguliwa kuwa rais wa ECOWAS, Juni, 4 2017.
Rais wa Togo Faure Gnassingbé ambaye amechaguliwa kuwa rais wa ECOWAS, Juni, 4 2017. ISSOUF SANOGO / AFP

Rais wa Togo Faure Gnassingbé ndiye rais wa sasa wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi Afrika Magharibi ECOWAS. Alichaguliwa siku ya Jumapili Juni 4 katika mkutano wa 51 wa viongozi wa nchi wanachama wa ECOWAS mjini Monrovia, nchini Liberia. Anachukuwa nafasi ya rais wa Liberia Ellen Johanson Sirleaf

Matangazo ya kibiashara

Faure NGnassingbe alitoa wito kwa ushirikiano zaidi na kupongeza maendeleo ya kiuchumi yaliofikiwa katika ukanda huo wa Afrika Magharibi, wakati ambapo moja ya maamuzi ya mkutano huo ni kujenga barabara kuu kati ya Abidjan na Dakar.

"Sasa tunahitaji kufanya kiwango kikubwa cha ubora kuelekea lengo letu moja, ambalo ni kulifanya jumuiya yetu kuwa ni ya wananchi wote kutoka mataifa wanachama wa ECOWAS. Itatubidi bila kuchelewa kuondoa vikwazo vya mwisho vinavyowakabili wananchi wetu, kuwawezesha vijana wetu kwa kuhimiza maendeleo yao kiuchumi katika ukanda huu, kuwaendeleza wafanyabiashara wetu, kutumia uwezo wetu wa idadi ya watu , kuzingatia kilimo na viwanda ... changamoto nyingi ambazo tunatakiwa kwa pamoja kukabiliana nazo kwa minajili ya maendeleo ya watu wetu, " alisema rais wa Togo.

Mfalme wa Morocco Mohammed VI hakuhudhuria mkutano huo, baada ya kufuta ziara yake katika dakika za mwisho, kwa sababu ya kuwepo kwa mgeni mwingine maalum: Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu. Ziara ambayo kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Israel ni heshima kwa krudi kwa uhusiano wa kidiplomasia katia ya Israel na bara la Afrika.

"Israel imerejea Afrika na imerejea upya Israeli. Nina matumaini kwamba tunaweza kufikia mikataba miwili muhimu kwa kuimarisha ushirikiano wetu. Israel inafungua tume mbili mpya za kibiashara: moja katika Afrika Magharibi na nyingine katika Afrika ya Mashariki ili kuimarisha biashara kati ya nchi zetu, " Benyamin Netanyahu, amesema.

Niger iliwakilishwa katika mkutano wa Monrovia na balozi wake. Kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu na serikali ya Niger, rais wa nchi hiyo Mahamadou Issoufou amekataa mwaliko kutokana na kuwepo kwa Waziri Mkuu wa Israel. Niger haina uhusiano wa kidiplomasia na Israel kwa miaka kadhaa.

Ujumbe wa watu zaidi ya 200 walihudhuria katika mkutano wa Monrovia, ambapo ahadi nyingi zilitolewa na mikutano kadhaa baina ya Israel na nchi hizo ilifanyika. Kwa mjibu wa Emmanuel Nashon, msemaji wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel inaweza kuleta mambo mengi barani Afrika. "Katika nyanja ya kilimo, maji, teknolojia ya juu pia katika nyanja ya usalama, nadhani kuna mazungumzo muhimu ambayo yanafanyikakati ya Israel na nchi za Afrika Magharibi, , ameongeza Bw Nashon.

Mpango wa uwekezaji wa "Dola bilioni 1" katika nishati mbadala ilitangaza katika mkutano huo. Changamoto kwa Israel ni kuimarisha mahusiano ya kiuchumi, lakini pia kukabiliana na nchi za Afrika zinapiga kura "dhidi ya Israel" katika taasisi za kimataifa.