NIGERIA-BUHARI-AFYA

Aisha Buhari: Rais Buhari anaendelea kupata nafuu

Rais Muhammadu Buhari Septemba 20,2016 wakati alipokua ziarani New York.
Rais Muhammadu Buhari Septemba 20,2016 wakati alipokua ziarani New York. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anaendelea kupata nafuu, wakati huu akiendelea kypata matibabu jijini London nchini Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Hakikisho hilo limetolewa na mkewe Bio.Aisha Buhari ambaye amerejea jijini Abuja baada ya kumtembelea mumewe hospitalini.

Rais Buhari alikwenda nchini Uingereza mwezi mmoja uliopita kuendelea kupata matibabu, ikiwa ni mara yake ya pili kufanya hivyo.

Mwanzoni mwa mwezi huu serikali ya Nigeria ilisema hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu afya ya rais Muhammadu Buhari anayeendelea kupata matibabu nchini Uingereza.

Waziri wa Habari nchini Nigeria Lai Mohammed, alitoa hakikisho hilo jijini Abuja, wakati huu raia wa Nigeria wakiendelea kujiuliza kuhusu hali ya afya ya kiongozi wao ambaye hajarejea nchini kwa muda wa wiki tatu sasa tangu alipokwenda nchini Uingereza.

Buhari mwenye umri wa miaka 74, kwa kipindi kirefu mwaka huu amekuwa jijini London kuonana na madakatari wake.

Mkewe Bi.Aisha Buhar aliondoka jijini Abuja mwanzoni mwa mwezi huu kwenda jijini London baada ya kukanusha madai kuwa mumewe alikuwa amezidiwa na ingekuwa vigumu kwake kuongoza.

Viongozi wa dini nchni Nigeria wameendelea kumwombea rais Buhari, ambaye wakati akiondoka jijini Abuja wiki tatau zilizopita, aliwaambia wananchi wa taifa hilo kuwa Madaktari wake ndio watakaoamua ni lini atarejea nyumbani.